IQNA

Waziri wa Utamaduni wa Iran:

Nakala milioni moja za Qur’ani kuchapishwa mkabala wa kila Qur’ani inayochomwa moto

18:54 - September 14, 2010
Habari ID: 1994074
Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa nakala milioni moja za Qur’ani Tukufu zitachapishwa hapa nchini mkabala wa kila Qur’ani inayochomwa moto au kuvunjiwa heshima.
Sayyid Muhammad Husseini ameyasema hayo leo katika maandamano makubwa ya wananchi wa jiji la Tehran waliokuwa wakipinga kitendo cha kuchomwa moto na kuvunjiwa heshima Qur’ani nchini Marekani. Waziri wa Utamaduni wa Iran ameashiria aya aya ya 39 ya suratul Tauba inayosema: "Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kutimiza nuru yake ijapokuwa makafiri wanachukia" na akasema wale wanaodai kushika bendera ya kutetea haki za binadamu na uhuru ni kwa nini wanavunjia heshima matukufu na kitabu cha Waislamu bilioni moja na nusu ambacho kinamtukuza na kumuenzi pia Nabii Issa Masia?
Maandamano ya kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Marekani yamehudhuriwa na makari wa Qur’ani na jumuiya na taasisi mbalimbali hapa nchini.
Maandamano kama hayo yameendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali nchini Iran. 655132
captcha