IQNA

Jumuiya ya nchi za Kiislamu yamkosoa Kamishna Muu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa

19:13 - September 14, 2010
Habari ID: 1994075
Mwakilishi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amemkosoa Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo kwa kupuuza suala la kuchomwa moto Qur’ani nchini Marekani.
Zamir Akram ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha 15 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kwa niaba ya nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC amemkosoa vikali Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa kupuuza tukio la kuchomwa moto kitabu kitakatifu cha Qur’ami nchini Marekani akisema kuwa kiongozi huyo hakuashiria hata kidogo suala hilo katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho. Amesema kuwa kitendo cha kasisi wa Marekani cha kuainisha tarehe 11 Septemba kuwa ni siku ya kimataifa ya kuchomwa moto Qur’ani ni kielelezo cha ubaguzi wa kidini na dharau dhidi ya matukufu ya dini nyingine. Amesisitiza kuwa kutoashiriwa suala hilo katika hotuba ya ufunguzi ya kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ni suala ambalo haliwezi kukubaliwa.
Mwakilishi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya ubaguzi na ukatili dhidi ya Uislamu hakupaswi kupufumbiwa macho. 654502
captcha