Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kituo cha Darul Qur'ani al Karim cha mji wa Nasiriyya nchini Iraq Ra'd Adnan al Nasiri katika mazungumzo yake na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa IQNA. Amesema kuwa taasisi za jumuiya zinazoshughulikia masuala ya Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu zinapaswa kubainisha hakika na mafundisho halisi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu Qur'ani Tukufu kwa njia ya kuitisha makongamano na vikao vya Qur'ani na kujibu kitendo hicho kiovu kupitia njia hiyo.
Amesema kwa msingi huo kituo cha Darul Qur'ani cha mji wa Nasiriyya kimepanga kuitisha mahfali ya Qur'ani katika siku chache zijazo ili kujibu kitendo cha Wakristo wenye misimamo mikali wa Marekani cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Amesema kuwa taasisi na jumuiya mbalimbali za Iraq zimelaani vikali uamuzi wa Kasisi Terry Jones wa Marekani wa kutaka kuchoma moto Qur'ani siku ya tarehe 11 Septemba. 656892