Kasisi Sabah Michael wa mjini Baghdad amesema kuwa Wakristo wote wanapinga vikali kitndo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu na wanaitambua Qur'ani kuwa ni kitabu kitakatifu cha mbinguni na kinachopaswa kuheshimiwa.
Amesema kuwa kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani kimewakasirisha mno Wakristo kabla hata ya Waislamu kwani kuivunjia heshima Qur'ani ni kumvunjia heshima Mwenyezi Mungu Mtukufu na neno lake.
Vilevile askofu Tania Jalal wa Iraq amesisitiza kuwa Wakristo wanalaani kitendo cha kuchomwa moto nakala za kitabu cha Qur'ani kwa kutumia kisingizio chochote kile na kwamba kitendo hicho ni dharau kwa matukufu ya Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu kote duniani. Kasisi Jalal amesema dini na mafundisho ya Kikristo yanapinga kitendo hicho kiovu.
Kasisi William George wa Iraq pia ameeleza kusikitishwa na kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani na kuongeza kuwa mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani yalitekelezwa na watu wenye misimamo mikali na wala hayana mfungamano wowote na Waislamu. Kasisi George amesema Qur'ani tukufu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu kinachosisitiza juu ya kuheshimiwa dini na kulindwa damu na heshima za watu wote. 656864