Kwa mujibu wa gazeti la Kuwait la Anbaa mashindano hayo ambayo yatafanyika katika makundi mawili ya wanaume na wanawake yameandaliwa na Idara Kuu ya Vijana na Masuala ya Michezo ya Kuwait kwa ushirikiano wa Idara ya Masuala ya Qur'ani Tukufu ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait.
Jassim Ya'qub naibu mkuu wa idara iliyotajwa ya vijana amesema kuhusu suala hilo kwamba, mashindano hayo yatachangia pakubwa katika kuwajenga vijana na shakhsia zao za baadaye kwa misingi ya thamani za Kiislamu na Qur'ani.
Amesema, pia yatasaidia katika kuhudumia Qur'ani na kueneza utamaduni wa Kiislamu katika jamii ya Kuwait. 657754