IQNA

Mwandishi mashuhuri wa Kimarekani awaomba radhi Waislamu

17:31 - September 20, 2010
Habari ID: 1997955
Mwandishi mashuhuri anayeandika makala katika gazeti la New York Times Nicholas Christopher amewaomba radhi Waislamu kote duniani hususan Waislamu wa nchi hiyo kutokana na kuongezeka wimbi la ubaguzi dhidi ya Waislamu na propaganda chafu dhidi ya dini hiyo nchini Marekani.
Katika makala yake ya jana kwenye gazeti la New York Times iliyofuatia kuzidi kwa ubaguzi wa makundi yenye misimamo mikali dhidi ya matukufu ya Kiislamu nchini Marekani iliyobeba anwani ya 'Ujumbe kwa Waislamu', Nicholas Christopher aliomba radhi kutokana na wimbi kubwa la chuki na wendawazimu kipofu unaowalenga Waislamu nchini humo.
Amesema inasikitisha kwamba Wamarekani wanashuhudia Waislamu wenye misimamo ya wastani wakikabiliwa na hatari na vitisho na Waislamu wasiokuwa na hatia wanafananishwa na magaidi.
Katika makala hiyo mwandishi huyo mashuhuri wa Marekani ameelezea kusikitishwa na uamuzi wa kasisi mwenye misimamo ya kufurutu mipaka wa Kikristo Terry Jones wa kutaka kuchoma moto kitabu kitukufu cha Qur'ani na amaeandika kuwa: "Ninataka kuomba radhi kutokana na hatua hiyo ya kufurutu mipaka na inapaswa kueleweka kwamba misimamo mikali ya kufurutu mipaka itafuatiwa na misimao mfano wake." 659171
captcha