IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake kufanyika Kuwait

13:58 - September 21, 2010
Habari ID: 1998619
Mashindano ya tano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la 'Mama Kigezo' makhsusi kwa ajili ya wanawake yatafanyika tarehe 16 Oktoba katika mskiti mkuu wa Kuwait.
Mashindano hayo yanasimamiwa na Taasisi ya Mama Kigezo ya Kuwait kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu ya Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo.
Farija al Ahmad Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Kigezo amesema kuwa wanawake wa Kuwait wana fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano hayo hadi kufikia tarehe Mosi Oktoba.
Amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika nyanja mbalimbali za kuhifadhi Qur'ani na kwamba washindi watatunukiwa zawadi za kati ya dinari 500 hadi 100 za Kuwait.
Farija al Ahmad amesema miongoni mwa malengo ya mashindano hayo ni kuzidisha maarifa ya kidini na kiutamaduni ya wanawake na kuimarisha uhusiano wa wananchi na Qur'an na vilevile kulea kizazi kipya kwa mujibu wa mafundisho na thamani za Qur'ani. 659547

captcha