Sherehe za kuwatunza washindi hao zilihudhuriwa na Khalid al Jundi, mhubiri mashuhuri wa Kiislamu na mkuu wa kanali ya televisheni ya satalaiti ya Azhari. Mashindano hayo ya Qur'ani ya walemavu wa akili ni ya kwanza kufanyika katika ulimwengu wa Kiislamu
Khalid al Jundi amesema kuwa televisheni moja ya Misri ina mpango wa kuanzisha kampeni ya misaada kwa mahafidhi wa Qur'ani wenye ulemavu wa akili ambayo itawawezesha kuhifadhi Qur'ani nzima.
Amesema kuwa ratiba nyingine za mpango huo ni kuwalea walemavu wa akili, kuwatayarishia maisha bora na fursa ya kupata elimu na malezi.
Mashindano hayo ya kwanza ya kitaifa ya Qur'ani ya walemavu wa akili yalifanyika mwezi uliopita chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri. 659558