Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, Muhammad Salim al-Aufi, mkuu wa kamati inayoandaa kongamano hilo ambaye pia ni katibu mkuu wa Chapa ya Qur'ani ya Mfalme Fahd amesema kuhusiana na suala hilo kuwa wasanii walio na hamu ya kushiriki katika kongamano hilo wana muda wa hadi kufikia tarehe 9 Oktoba wawe wameshawasilisha kazi zao za sanaa kwa kamati hiyo.
Kongamano hilo linafanyika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuwashukuru wanakaligrafia na kuenzi nafasi yao katika kuhudumia Qur'ani Tukufu. Vikao kadhaa vya hotuba na masomo vitafanyika pembeni ya kongamano hilo katika kituo hicho cha uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd. 659651