IQNA

Nuskha mbili adimu za Qur'ani zahifadhiwa katika Chuo cha Williams nchini Marekani

12:51 - September 23, 2010
Habari ID: 1999871
Nuskha mbili adimu za Qur'ni Tukufu zinahifadhiwa katika maktaba ya Chuo cha Williams katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani. Hayo yamesemwa na Win G. Hammond mmoja wa wakuu wa chuo hicho.
Kwa mujibu wa tovuti ya berkshireeagle Hammond amesema kuwa moja ya nuskha hizo ambayo ni ya karne ya 19 na inayohusiana na utawala wa Othmania ilipelekwa katika maktaba hiyo miezi michache iliyopita.
Ameendelea kusema kuwa kitabu hicho ambacho kina urefu wa sentimita 15 na upana wa sentimita 10 kimeandikwa kwa maandishi ya kuvutia ya mkono na kurembwa kwa dhahabu. Amesema nuskha ya pili ambayo ilipelekekwa kwenye maktaba hiyo miaka kadhaa iliyopita pia imerembwa kwa sanaa ya kuvutia ya kaligrafia na dhahabu.
Inasemekana kuwa uandishi wa Qur'ani hiyo ambao ulitimia mjini Tehran ulimalizika mwaka 1833.
Win Hammond ameashiria matukio ya hivi karibuni ya kujengwa msikiti mjini New York na kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Marekani na kuelezea matumaini yake kwamba kwa kuonyesha umma Qur'ani hizo mbili adimu chuo hicho kitachangia juhudi za kuwafahamisha watu mafundisho ya Qur'ani. 660969
captcha