Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, masomo hayo ambayo yatawajumuisha zaidi ya wahubiri na maimamu 910 kutoka mikoa tofauti ya Misri yatafunguliwa rasmi na Mahmoud Hamdi Zaqzouq, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri.
Uchunguzi wa masuala ya uhubiri, kubadilishana uzoefu wahubiri kuhusiana na masuala ya kidini, kuleta mwamko wa kidini katika jamii kwa kuzingatia zama na mitazamo ya wahubiri na maimamu wa swala za jamaa kuhusiana na shughuli za uhubiri ni masuala yatakayojadiliwa katika vipindi hivyo vya masomo.
Katika kipindi cha masomo hayo, washiriki wanatazamiwa kukutana na wakuu, wataalamu wa maarifa ya Kiislamu pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Masomo ya Kidini cha al-Azhar. 662562