Mtandao wa habari wa Leblover umeripoti kuwa nakala hiyo ya zamani ya Qur'ani Tukufu ina kurasa 22 na imeandikwa kwa hati za Hijazi. Ukurasa huo una urefu wa sentimita 33 na upana wa sentimita 23 na bei yake inakadiriwa kuwa karibu dola laki mbili na 37 elfu.
Kituo cha minada cha Christy cha London hakikuashiria ukurasa huo wa Qur'ani ya zamani umepatikana wapi na unamilikiwa na nani.
Utafiti na chunguzi za kielimu zinaonyesha kuwa nakala zilizoandikwa katika zama za awali za Uislamu ziliandikwa kwa hati za Hijazi na bila kuwa na irabu. Herufi za nakala hizo pia hazikuwa na nukta juu au chini yake. 663640