Mwanachama mmoja wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Misri amesema kuwa matamshi ya dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu yaliyotolewa na Kasisi al Anba Bishoy wa Misri yametolewa kwa uungaji mkono wa kanisa na Papa Shenouda III, Kiongozi wa Kanisa la Makopti ambaye ni maarufu kwa kuupiga vita Uislamu.
Muhammad Ammarah, mhakiki wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Misri amesema kuwa matamshi yaliyotolewa na Kasisi Bishoy dhidi ya Qur'ani si mtazamo wake binafsi bali yanawakilisha mtazamo wa kanisa la Makopti na Papa Shenouda III, Kiongozi wa Kanisa hilo. Amesisitiza kuwa ukwelli huo unaonekana wazi katika historia ya kiongozi huyo.
Bwana Ammarah amesema kuwa Waislamu wamekwisha jeruhiwa na matamshi ya kibaguziya Papa Shenouda ambaye miaka mingi iliyopita alikuwa akidai kwamba Waislamu ni wageni tu nchini Misri.
Amesema Papa Shenouda ni mwanachama wa jumuiya inayoamini kwamba ardhi yote ya Misri ni nchi ya Makopti iliyoghusubiwa na Waarabu na Waislamu katika karne ya 14 Miladia. 665691