Kwa mujibu wa tovuti ya Ruqayah.net, ujumbe huo ambao pia umemjumuisha Mustafa as-Swarraf, msomaji wa kimataifa wa Qur'ani, umekutana na kubadilishana mawazo na wakuu wa kituo hicho kuhusiana na njia za kubadilishana uzoefu kuhusiana na shughuli na ratiba za Qur'ani.
Katika mazungumzo hayo, wakuu wa kituo hicho cha Qur'ani waliwapa wageni wao zawadi ya vitabu, majarida na cd kadhaa za shughuli za kituo hicho.
Ujumbe huo wa pia umekutana na kundi la wasomaji kasida la al-Ghadir la mjini Qum na kubadilishana nalo uzoefu wa kisanaa katika uwanja wa masuala ya kidini. 666515