IQNA

Mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani na hadithi za Mtume (saw) yafanyika Indonesia

19:13 - October 03, 2010
Habari ID: 2005944
Mshindano ya kimataifa ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur'ani na hadithi za Bwana Mtume (saw) yalianza jana Jumamosi huko Jakarta mji mkuu wa Indonesia.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la Iqtiswadiyyah, washiriki 87 wanashiriki katika mashindano hayo kama wahifadhi wa Qur'ani na wengine 38 katika kuhifadhi hadithi za Mtume (saw).
Washiriki wanatoka katika nchi 16 za Asia na eneo la Pacific.
Kuwashajiisha vijana wa Asia wahifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu pamoja na kuhifadhi hadithi za Bwana Mtume (saw) na vilevile kuimarisha mfungamano wa vijana hao na Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni baadhi ya malengo ya kufanyika mashindano hayo.
Sherehe za kushukuriwa na kuzawadiwa washindi wa mashindano hayo zitafanyika kesho Jumatatu ambapo rais wa Indonesia anatazamiwa kushiriki. 667421
captcha