IQNA

Familia za Qatar kushiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani

17:07 - October 05, 2010
Habari ID: 2007219
Mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani ambayo yanatazamiwa kufanyika nchini Qatar chini ya anwani ya 'Familia Hafidh' na ambayo ni mashindano maalumu kwa ajili ya familia za nchi hiyo, yamepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq, Ibrahim Aal Ibrahim mkuu wa baraza la uongozi la Darul Qur'ani ya Qatar amesema kuhusiana na jambo hilo kwamba familia za nchi hiyo zina fursa ya kati ya tarehe 10 hadi 17 Oktoba kwa ajili ya kusajili majini yao kwa lengo la kushiriki katika mashindano hayo.
Amesema kamati inayosimamia mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka ina lengo la kuyafanya kuwa ya kimataifa. Ibrahim Aal Ibrahim amesema maana ya 'familia hafidh' ni kushajiisha mmoja wa wazazi ama mama au baba na wana wao waweze kuhifadhi Qur'ani na hatimaye kushiriki katika moja ya mashindano hayo.
Amesema lengo kuu la kuandaliwa mashindano hayo ni kuhamasisha familia zihifadhi Qur'ani na kuichukulia kuwa chanzo cha kubuniwa sheria zinazolinda haki na kusimamia majukumu yao yote maishani. 668669
captcha