IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani Tanzania wazawadiwa

10:03 - October 17, 2010
Habari ID: 2013872
Washindi wa mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Tanzania wametunukiwa zawadi katika mji mkuu wa nchi hiyo Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu, mashindano hayo yamefanyika kwa himaya ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ikishirikiana na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani Tanzania na yalikuwa na washiriki 364.
Mashindano hayo yalikuwa na viwango vitano vya kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi Juzuu 25 za Qur'ani Tukufu, kuhifadhi juzuu 20 za Qur'ani Tukufu, kuhifadhi Juzuu 10 za Qur'ani Tukufu na Juzuu 3 za Qur'ani Tukufu.
Hafla ya kuwatunuku zawadi washindi iliyofanyika Jumamosi tarehe 24 Oktoba, ilihudhuriwa na maafisa wa serikali ya Tanzania, maulama na shakhsia wa kidini na Qur'ani wa nchi hiyo.
Waliohutubia hafla hiyo walipongeza Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa juhudu zake za kuandaa mashindano hayo ya Qur'ani ambayo yametajwa kuwa hatua muhimu katika kuuhudumia Uislamu na Waislamu na kuzingatia Qur'ani kutukufu pamoja na kueneza utamaduni wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu duniani. 676130
captcha