Akizungumzia suala hilo hivi karibuni huko Kuwait, Ayatullah Dibaji alisisitiza juu ya umuhimu wa kubainishwa wazi misingi na matawi ya dini yanayowaunganisha Mashia na Masuni. Akizungumza mbele ya wawakilishi wa vyombo vya habari na idadi kadhaa ya wanazuoni, Ayatullah Dibaji amesema kuwa kuzusha fitina miongoni mwa Waislamu na kuwagawa katika makundi ni kufri kubwa zaidi kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu. Amesema, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikihubiri fitina na siasa za kuwatenganisha Waislamu kwa kusisitiza juu ya hitilafu ndogondogo zilizopo kati ya Waislamu.
Ayatullah Dibaji ambaye pia ni imamu wa Msikiti wa Zeinul Abedeen wa Kuwait amesema Mtume Mtukufu (saw) alitumwa na Mwenyezi Mungu ili aje kukamilisha misingi ya thamani na fadhila za kimaadili na kiakhlaqi na kwamba Waislamu wanapasa kuwadhihirishia sura halisi ya Uislamu wafuasia wa dini nyinginezo kwa kulinda umoja na mshikamano miongoni mwao. 678260