Masomo hayo yamepangwa kuendelea kwa muda wa miezi miwili. Akizungumzia suala hilo Ra'd Adnan an-Nasiri, mkuu wa taasisi hiyo ya Qur'ani ya Nasiriyya amesema katika hatua ya kwanza, masomo hayo yatawashirikisha wafanyakazi wa idara za masomo na maelezi, umeme, afya na wafanyakazi wa idara ya meya wa mji huo.
Amesema masomo hayo yatajumuisha kanuni za usomaji na hifdhi ya Qur'ani Tukufu. Amesema wafanyakazi wamefurahishwa na masomo hayo na kwamba wamekuwa wakijiandikisha kwa wingi ili kushiriki kwenye masomo hayo. 678406