IQNA

Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar yatahadharisha viwanda vya uchapishaji wa Qur'ani vya Misri

18:52 - October 20, 2010
Habari ID: 2016841
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar imevitahadharisha viwanda vya uchapishaji Qur'ani vya Misri kwamba iwapo vitachapisha nakala za Qur'ani zenye makosa ya kiuchapishaji zitanyang'anywa kibali.
Taasisi hiyo imesisitiza kuwa malalamiko mengi yamewasilishwa kuhusu makosa ya kimaandishi ya nakala za Qur'ani na kwamba tangu sasa taasisi yoyote ya uchapishaji itakayopatikana na makosa kama hayo itanyang'anywa kibali cha uchapishaji.
Afisa mmoja wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiislamu ya al Azhar amesema kuwa Sheikh Mkuu wa al Azhar Ahmad al Tayyib anachunguza uwezekano wa kuanzisha kiwanda cha uchapishaji wa nakala za Qur'ani Tukufu kwa ajili ya kuzuia uchapishaji wa nakala zenye makosa ya kimaandishi. 678935

captcha