IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani ya mjini London wazawadiwa

13:49 - October 23, 2010
Habari ID: 2017623
Washindi wa mashindano ya Qur'ani ya Kituo cha Utamaduni na Kiislamu cha London leo Jumamosi watazawadiwa zawadi nono kutokana na kushiriki kwao katika mashindano hayo.
Kwa mujibu wa tovuti ya kituo hicho, hafla ya kutolewa zawadi hizo itaanza mara tu baada ya kumalizika swala ya adhuhuri katika kituo hicho.
Mashindano hayo yaliyofanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na yaliyodhaminiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia, yalifanyika katika hatua kadhaa za kuhifadhi juzuu moja, tano, kumi, ishirini na thelathini za Qur'ani Tukufu.
Lengo la kufanyika mashindano hayo lilitajwa kuwa ni kuwashajiisha Waislamu na hasa vijana wahifadhi Qur'ani na kujishughulisha na masuala ya Kiislamu na Qur'ani maishani. 679937
captcha