IQNA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bonn asisitiza juu ya kutarjumiwa Qur'ani kwa lugha mbalimbali

13:51 - October 30, 2010
Habari ID: 2022081
Mhadhiri mstaafu wa lugha za Kisemiti na utafiti wa masuala ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Bonn nchini Ujerumani amesisitiza juu ya udharura wa kutarjumiwa Qur'ani kwa lugha mbalimbali licha ya kukiri kwamba ni muhali kuweza kutarjumu kitabu hicho kikamilifu.
Stephan Wayld amesema katika kikao kilichotayarishwa na Kitengo cha Utafiti wa Mashariki ya Kati cha Chuo Kikuu cha Harvard kwamba kitabu kitakatifu cha Uislamu hakiwezi kutartumiwa kikamilifu na inavyotakikana kwa lugha nyingine na kinapotarjumiwa muujiza wa fasihi yake hutoweka.
Stephan Wayld ameongeza kuwa swali gumu katika kadhia hii ni jinsi ya kuweza kutarjumu Qur'ani Tukufu na wakati huo huo kulinda maana na ubora wa kifasihi wa kitabu hicho.
Mhadhiri huyo Mmarekani wa Chuo Kikuu cha Bonn amesisitiza juu ya kutarjumiwa Qur'ani Tukufu na wakati huo huo amekiri kwamba ni muhali kuweza kutarjumu kikamilifu maana ya kitabu hicho kwa lugha nyingine. 684654
captcha