IQNA

Chuo Kikuu cha London, mwenyeji wa masomo ya kufahamu tafsiri ya Qur'ani

11:39 - October 31, 2010
Habari ID: 2022609
Masomo ya muda mfupi ya kujifunza tafsiri ya Qur'ani Tukufu yataanza kutolewa katika Chuo Kikuu cha Sanaa cha mjini London Uingereza Jumamosi ya Tarehe 20 Novemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya IIDR masomo hayo yanadhaminiwa na Chuo cha Utafiti wa Qur'ani cha Uingereza BAQS kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Sanaa cha Uingereza.
Mambo yatakayojadiliwa katika masomo hayo ya siku moja ni pamoja na maana na umuhimu wa tafsiri ya Qur'ani, Tafsiri katika mtazamo wa historia, vyanzo na aina ya tafsiri, tafsiri za Qur'ani zenye itibari, wafasiri wa Qur'ani, tafsiri katika karne ya 20 na umuhimu wa kufahamu lugha ya Kiarabu katika kufasiri Qur'ani.
Sheikh Hassan al-Banna, mku na mwanzilishi wa Taasisi ya Ustawi na Utafiti wa Kiislamu IIDR na aliyehitimu masomo ya fiqhi katika Chuo Kikuu cha Kidini cha al-Azhar ndiye atakayesimamia masomo hayo. Mwanazuoni huyo pia ameandika na kutarjumu vitabu vingi vya Kiislamu.
Chuo Cha Ustawi na Utafiti wa Qur'ani cha Uingereza BAQS ni taasisi muhimu iliyo na ratiba maalumu na madhubuti ya utafiti wa Qur'ani ukiwemo utoaji wa masomo ya muda mfupi ya tafsiri ya Qur'ani kila mwezi.
Tafsiri ya Qur'ani ni moja ya masomo muhimu ya Kiislamu ambayo yamekuwa na athari muhimu katika historia ya mwanadamu. 685108
captcha