IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani ya Bunge la Iran wazawadiwa

10:28 - November 09, 2010
Habari ID: 2028196
Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya wafanyakazi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wametunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Novemba 8.
Sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa sala wa Bunge na kuhudhuriwa na Naibu Spika wa Bunge la Iran Sheikh Abu Turabifard.
Mkuu wa Chuo cha Qur'ani cha Bunge amesema mashindano hayo ya nane yamepokelewa vizuri na wafanyakazi pamoja na familia zao.
Amesema mashindano hayo yalikuwa na washiriki 200 katika viwango vya tajweed, tartee na hifdh. Aidha kulikuwa na mashindano kuhusu sala , adhana na usomaji vitabu. Washiriki 30 waliibuka washindi na kutunukiwa zawadi.
Naibu Spika wa Bunge la Iran Sheikh Abu Turabifard ametoa salamu za heri na fanaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ndoa ya Imam Ali bin Abi Twalib AS na Bibi Fatima Zahra SA ambayo huadhimishwa tarehe Mosi Dhul Hijja. Sheikh Abu Turabifard amefafanua kuhusu majukumu ya mume na mke katika familia. 691242

captcha