Kwa mujibu wa gazeti la Hurriyet linalochapishwa nchini Uturuki, Idara ya Wakfu ya Uholanzi kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kidini ya Hague ina lengo la kusambaza nakala hizo miongoni mwa Waislamu na wasio Waislamu kwa mnasaba wa Jumuiya ya Masuala ya Kidini ya Uturuki kuutangaza mwaka huu wa 2010 kuwa mwaka wa Qur'ani Tukufu.
Nakala hizo zilianza kuchapishwa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na jumuiya iliyotajwa ya Hague imeamua kusambaza nakala zilizochapishwa tayari miongoni mwa watu wa Uholanzi.
Lengo la hatua hiyo limetajwa kuwa ni kupambana na kuenea fikra za chuki na uadui dhidi ya Uislamu pamoja na kueneza mafundisho halisi ya Uislamu miongoni mwa raia wa nchi za Ulaya. 697602