Ripoti za polisi zinasema kuwa zaidi ya Waislamu 300 waliandamana mbele ya jengo la Halmashari ya Jiji la Athens wakitangaza upinzani na malalamiko yao dhidi ya kitendo hicho.
Kufuatia malalamiko hayo, viongozi wa mji wa Athens wamekadhibisha habari kwamba afisa wa pilisi ya nchi hiyo amechana na kurarua nakala ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani baada ya kumtia nguvuni raia mmoja wa Misri.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu nchini Ugiriki Naeem al Qadur anasema hali ya Waislamu nchini humo imekuwa mbaya sana. Ameongeza kuwa Jumanne iliyopita watu kadhaa wasiojulikana walikuwa na nia ya kuwafungia Wahajiri 40 wa Kibangladeshi ndani ya msikiti na kuwachoma moto.
Waislamu wa Athens pia walishambuliwa siku ya Idul Haji na kusumbuliwa na wenyeji wa Kigiriki.
Karibu Waislamu laki moja kutoka nchi za Kiarabu, Kiafrika na Asia wanaishi na kufanya kazi katika hali na mazingira mabaya mjini Athens, Ugirki. 697618