IQNA

Tahadhari ya Saudi Arabia kuhusu kuingizwa nchini humo Qur'ani zilizo na kasoro ya chapa

16:15 - November 22, 2010
Habari ID: 2035990
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia imetahadharisha juu ya kuingizwa nchini humo nakala za Qur'ani zilizo na kasoro za chapa au upungufu na ukaririwaji wa aya zake tukufu.
Kwa mujibu wa gazeti la kimataifa la Dar al-Hayaat, wizara iliyotajwa imelazimika kutoa tahadhari hiyo baada ya taasisi moja ya usambazaji ya Saudi Arabia kutawanya nchini humo nuskha hizo zilizo na kasoro zilizochapishwa nje ya nchi hiyo. Nuskha hizo zina baadhi ya aya zilizofutwa au sura zilizokaririwa zikiwemo za Aal Imran na Nisaa.
Wizara hiyo imezitaka idara zote za ushuru katika viwanja vya ndege bandarini na njia nyinginezo za kuingilia nchini humo kuchukua tahadhari ya ziada ili kuzuia kuingizwa nchini humo nakala kama hizo zilizo na kasoro.
Maafisa wa nchi hiyo wanasema kuwa kwa bahati mbaya baadhi ya nakala hizo zimetawanywa katika misikiti na maeneo mengine ya nchi hiyo jambo ambalo limeamsha hasira na malalamiko ya watu nchini humo. 699566
captcha