IQNA

Nakala zilizopotoshwa za Qur’ani zakusanywa nchini Misri

10:08 - November 27, 2010
Habari ID: 2037873
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri ikishirikiana na vyombo vya usalama nchini humo imekusanya karibu nakala 4000 za Qur’ani Tukufu ambazo zimepotoshwa kwa kufutwa baadhi ya aya za sura za kitabu hicho na zina makosa makubwa na kinahau, lugha na maandishi.
Wizara ya Wakfu ya Misri pia imekusanya nakala nyingine karibu 3500 za Qur’ani ambazo baadhi ya aya zake zimefutwa na nyingine kupotoshwa.
Ripoti zinasema kuwa katika nakala hizo zilizopotoshwa, aya zinazohusiana na jihadi, uharamu wa pombe na vileo, historia ya Bani Israel na visa vyao vimepotoshwa.
Nakala hizo za Qur’ani hazikuwa na ruhusa ya kuchapishwa kutoka vyombo husika na zilikuwa zikitolea kwa wananchi wa Misri katika maktaba za umma na maduka ya kuuza vitabu kabla ya kukusanywa na Wizara ya Wakfu ya Misri ikishirikiana na vyombo vya usalama.
Katika upande mwingine vyombo vya usalama vya Misri vimetangaza kuwa nakala hizo zenye makosa ya chapa na aya zilizopotoshwa hazikuchapishwa nchini humo na kwamba zimeingizwa Misri kutoka nje ya nchi kwa njia zisizokuwa za kisheria. 701681
captcha