Ali Bakhtiari, Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Zambia amesema masomo hayo ya muda wa miezi miwili yalimalizika Novemba 18 na yalikuwa na vikao 20 na yalifanyika katika Msikiti wa Imam Reza AS.
“Washiriki 20 walio na umri kati ya miaka 8-15 walifunzwa namna ya kusoma Qur'ani na walifanikiwa kuhifadhi surah 10 za juzuu Amma katika Qur'ani Tukufu”, amesema.
Ameongeza kuwa: “kama ilivyo katika nchi zingine za Afrika, Zambia imekuwa chini ya ushawishi wa utamaduni wa Kimagharibi lakini watu hawajaweza kupata suluhisho la matatizo ya kimaadili na ufisadi wa jamii katika mafundisho ya Kikristo na kwa hivyo wameigeukia Qur'ani”.
702229