Gazeti la al Khaleej limeandika kuwa nakala hizo za kitabu kitakatifu cha Qur’ani zitmetolewa kwa Kituo cha Ibn Taimiyya cha Togo, Jumuiya ya Utamaduni na Masuala ya Kiroho ya Taasisi ya Mayatima ya Burundi, kituo cha al Huda wal Nur cha Mauritius na Taasisi ya al Birr ya Senegal.
Makala hizo za Qur’ani ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya al Birr ya Imarati kwa ajili ya kuhifadhi na kutoa mafunzo ya Qur’ani kwa wanachuo na kulinda vituo vya Qur’ani na walimu wa kitabu hicho katika nchi za Kiafrtika.
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kuwalinda Walimu na Wanachuo ya Imarati Yusuf al Yatiim amesema kuwa Taasisi ya masuala ya kheri ya al Birr itaendele kufanya juhudi za kuhudumia kitabu kitakatifu cha Qur’ani.
Ameongeza kuwa nakala hizo za Qur’ani zitagawanywa katika misikiti, vituo vya elimu na vyuo vya Qur’ani Tukufu katika nchi zilizotajwa za Kiafrika. 703729