Maonyesho hayo ambayo yamedhaminiwa na idara inayosimamia Haram ya Imam Ali (as) yataendelea hadi siku ya Jumamosi Disemba Nne. Nuskha ya Qur'ani inayosemekana kuandikwa na Imam Ali (as) pamoja na ya Yaqut al-Mu'taswimi, mwandishi Qur'ani mashuhuri katika enzi za utawala wa Bani Abbas, ni miongoni mwa vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho hayo.
Nuskha zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo ni za kale, nadra na zilizoandikwa kwa hati tofauti za Kiarabu ikiwemo hati ya Kufi.
Maonyesho hayo ni ya kwanza ya aina yake nchini Iraq.
Ni muhimu kuashiria hapa kwamba hati za Qur'ani, athari, vitabu na nyaraka zinazohifadhiwa katika Haramu ya Imam Ali (as) zinarudi nyuma katika historia tokea karne ya kwanza hadi ya 14 Hijiria. 703200