Kikao cha kuchunguza njia bora za kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu, kanuni za lugha ya Kiarabu na sheria za Kiislamu kwa kizazi kipya cha Waislamu waliowachache nchini Uingereza kimepangwa kufanyika katika Kituo cha Kiislamu cha London.
Kwa mujibu wa ripoti za kituo hicho, kikao hicho kimepangwa kufanyika Jumpaili Disemba 5. Kikao hicho kitahudhuriwa na wasimamizi wa shule za Kiarabu za mjini London. Wakuu wa shule hizo wamepangiwa kujadili na kujibu maswali ya wazazi na wasimamizi wa wanafunzi wa kizazi kipya cha Kiislamu nchini Uingereza kuhusiana na masuala ya mafundisho ya Qur'ani Tukufu, lugha ya Kiarabu na sheria za Kiislamu.
Kituo cha Kiislamu cha London kimesema kuwa lengo la kuandaliwa kikao hicho ni kutoa mafunzo na malezi bora kwa kizazi cha Kiislamu ambacho hakina uwezo wa kusoma vyema Qur'ani wala kutambua vizuri misingi ya sheria za Kiislamu.
Kituo hicho kimesema kuwa kufanikiwa kwa jambo hilo kunahitajia ushirikiano mzuri wa familia za wanafunzi na wakuu wa shule za lugha ya Kiarabu mjini humo. 704281