Kwa mujibu wa gazeti la Peninsula linalochapishwa nchini Qatar, maneno hayo yamesemwa na Sheikh Muhammad Daniel katika mkutano wa Doha na kuongeza kuwa uadilifu na usawa ni msingi muhimu wa mafundisho ya Kiislamu ambao unapaswa kulindwa na kuheshimiwa katika kila hali na mazingira. Amesema thamani za Kiislamu kama vile uadilifu na upendo hazihusiani na wanadamu tu bali hata wanyama na mazigira yanapasa kunufaika na thamani hizo kutoka kwa Waislamu.
Sheikh Muhammad Daniel amesema ni kwa msingi huo, ndipo kila jambo linalodhuru mazingira likaharamishwa na dini hii ya mbinguni.
Akizungumza katika mkutano huo Chandra Mohan Dos wakili mkuu katika Mahakama Kuu ya India pia amesema kuwa mafundisho ya Kiislamu ni rahisi na mepesi mno kiasi kwamba yanafahamika na kila mtu. Amesema watu wote duniani wanafahamu vyema kuwa Uislamu unahubiri amani na upendo na kwamba watu wanaowatuhumu Waislamu kuwa ni magaidi wanaotumia mabavu hawawafanyii uadilifu Waislamu. 704410