Masomo hayo yanadhaminiwa na Kituo cha Masomo kwa ajili ya Ustawi wa Kibinadamu cha Mauritania. Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Mauritania Ami, masomo hayo ambayo yanawashirikisha watu 80 chini ya nara ya, 'Mimi Nimehifadhi Qur'ani Tukufu,' yataendelea kwa muda wa siku tatu.
Maudhi kama vile mbinu kadhaa za kuhifadhi Qur'ani, stratejia ya kuimarisha hifdhi na kanuni 19 za kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika masomo hayo.
Muhammad Amin, mkuu wa kituo kilichotajwa cha Mauritania amesema kwamba nchi hiyo inahitajia ustawi mkubwa wa kibinadamu ili kujiendeleza katika kila nyanja. Amesema lengo la masomo hayo ni kubadili fikra ya jamii ya nchi hiyo na kuishirikisha katika ujenzi bora wa taifa lililosimama juu ya misingi na thamani imara. 705551