Mashindano hayo yalifanyika mwezi mtukufu wa Ramadhani na yaliandaliwa na Radio Qur'an ya Lebanon inayofungamana na taasisi ya Dar-ul-Ifta nchini humo.
Hafla hiyo ilifanyika chini ya uongozi wa Sheikh Muhammad Rashid Qabbani, Mufti wa Lebanon katika Dar-ul-Ifta mjini Beirut ambapo washindi 30 walitunukiwa zawadi.
Mkurugenzi wa Radio ya Qur'an alitoa hotuba katika hafla hiyo na kutoa maelezo kuhusu vipindi vya radio hasa vile vilivyopangwa mwezi wa Ramadhani.
Mufti wa Lebanon amepongeza juhudi za Radio ya Qur'an katika kuwatunukia zawadi washindi.
Amesisitiza kuwa Radio Qur'an ya Lebanon ina nafasi muhimu katika kueneza ustaarabu tajiri wa Kiislamu unaolenga kumuongoza mwanaadamu kutoka kwenye giza na kumuelekeza kwenye nuru.
Mufti wa Lebanon ametoa wito kwa Waislamu kurejea katika mafunzo ya Qur'ani na thamani za juu za Kiislamu
709871