Hayo yamesemwa na Umar bin Abdullah bin Ali al Bariki, karii na mwakilishi wa Oman katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu nchini Iran. Ameiambia IQNA kwamba watu wasiokuwa na elimu ya kutosha hawapaswi kuruhusiwa kutangaza Uislamu na kazi hiyo inapaswa kufanywa na wasomi kupitia ratiba na kazi za kiutamaduni na kuchukua jukumu la kulingalia dini ya Kiislamu.
Umar al Bariki amesema kuwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ni medani ya kuonyesha uwezo wa kitabu hicho kitakatifu na kuongeza kuwa anakusudia kustawisha zaidi uwezo na kipawa chake cha tajwidi na kiraa katika mashindano ya sasa.
Ameashiria taathira ya mashindano kama hayo ya Qur'ani katika kuelewa tamaduni za nchi mbalimbali za Kiislamu na akasema washiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya Qur'ani watapata fursa ya kutambua tamaduni mbalimbali.
Mwakilishi huyo wa Oman katika mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu mjini Tehran amesema kuwa katika mashindano ya Qur'ani wawakilishi wa nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu wanakusanyika sehemu moja na kushindana katika kusoma Qur'ani ambacho ni kitabu kitakatifu cha Waislamu wote na sababu ya uongofu na ufanisi wa dunia na akhera, suala ambalo linaweza kuimarisha zaidi umoja na mshikamano wa Kiislamu. 710435