Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la al-Madina watafiti na wanafikra wa Kiislamu wanaweza kunufaika kwa kiwango kikubwa na adhama ya kielimu ya Qur'ani na sunna za Mtume Muhammad (saw) katika kutoa hoja zenye nguvu katika mazungumzo yao ya tamaduni mbalimbali na pia kwa lengo la kuimarisha wito wa Kiislamu katika pembe mbalimbali za dunia.
Amesema wanazuoni wa Kislamu wana jukumu la kuwahimiza shakhsia, wahadhiri, wanachuo na wanafunzi, taasisi za utafiti na kielimu pamoja na vituo vya uhubiri na utamaduni kuzingatia umuhimu wa kuandika na kuchapisha vitabu kuhusiana na suala la muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu.
Ameongeza kuwa kikao kijacho cha jumuiya hiyo ambacho kimepangwa kufanyika tarehe 11 hadi 14 Machi mwakani huko Istanbul Uturuki, kitajadili suala hilo la muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume (saw) katika nyanja mbalimbali za tiba, mazingira, nujumu, elimu ya anga, ardhi, sayansi ya bahari na utungaji sheria. 710950