Hayo ni kwa mujibu wa Muhammad Tuhir karii wa Qur'ani mwene umri wa miaka 27 ambaye atawakilisha Indonesia katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu nchini Iran.
Katika mahojiano na IQNA, Muhammad Tuhir ameongeza kuwa: "Mashindano haya yatakuwa fursa nzuri ya kuiga uwezo na mafanikio ya washiriki wengine na kwa njia hiyo kuimarisha uwezo wetu katika masuala ya Qur'an"
Karii huyo wa Qur'ani kutoka Indonesia amesema mashindano hayo yatakuwa fursa ya kuimarisha umoja miongoni mwa wanachuo Waislamu kote duniani.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yatafanyika mwezi ujao wa Januari katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.