Kituo cha habari cha MSN News kimeripoti kuwa nakala hiyo ya Qur’ani Tukufu ina urefu wa sentimita 2.5 na upana wa sentimita 1.7 na inahifadhiwa na Alimuddin Qadhi.
Kurasa za nakala hiyo ya Qur’ani zina rangi nyeupe na zina unene wa sentimita 0.6. Matini ya sura za nakala hiyo pamoja na maandishi ya kandokando yake ina urefu wa sentimita 1.9 na upana wa sentimita 1.3.
Nakala hiyo ya Qur’ani Tukufu ni moja kati ya nakala nadra mno za Qur’ani duniani zenye vipimo hivyo vilivyotajwa.
Alimuddin Qadhi anayemiliki makala hiyo ya Qur’ani kwa miongo mitano sasa alirithi kitabu hicho kutoka kwa babu yake aliyekuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa India. 712529