IQNA

Kongamano la Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani kufanyika Marseille

8:20 - December 19, 2010
Habari ID: 2049234
Kongamano la Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani Tukufu limepangwa kufanyika tarehe 15 Januari katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.
Kituo cha habari cha Umma-united kimeripoti kuwa kongamano hilo linafanyika kwa hima ya Jumuiya ya Wanachuo Waislamu wa Ufaransa (EMF) na litahudhuriwa na mwandishi mashuhuri wa Uturuki Haroun Yahya.
Msomi huyo atahutubia kongamano hilo kuhusu nyanja za muujiza wa Qur'ani Tukufu na nadharia ya mageuzi ya mwanadamu (The evolution theory) kama nadharia inayokwenda kinyume na mafundisho ya Uislamu.
Adnan Oktar anayetumia jila bandia la Haron Yahya alizaliwa mwaka 1956 mjini Ankara, Uturuki na kuhitimu chuo kikuu akiwa na shahada ya falsafa na sanaa. Alianza kuandika vitabu akiwa na umri wa miaka 24 na hadi sasa ameandika karibu vitabu 222 katika nyanja mbalimbali za falsafa, dini, sayansi na siasa.
Baadhi ya vitabu vya msomi huyo ni kama: Perished Nations, Signs of the End Times in Surat al Kahf, Wonders of Allah's Creation na Miracles of the Qur'an. 713716

captcha