Kwa mujibu wa tovuti ya Daily News, kufikia sasa zaidi ya wanafunzi 250 walio na umri wa kati ya mika 7 hadi 18 tayari wamejiandikisha kushiriki katika mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika katika kituo cha Islah katika mji wa Maharraq nchini humo. Sherehe ya kukabidhiwa zawadi washindi wa mashindano hayo itafanyika tarehe 6 Januari.
Mashindano hayo yanadhaminiwa na kituo cha Wahat al-Qur'an al-Karim kinachofungamana na Jumuiya ya al-Islah kwa ushirikiano wa Taasisi ya Bima ya Kiislamu, kwa lengo la kuhuisha thamani za Kiislamu, kushajiisha shughuli za Kiislamu na kuwashawishi vijana wahifadhi Qur'ani Tukufu.
Mwaka jana mashindano hayo yaliwashirikisha washindani 200 kutoka shule za msingi 60 za Bahrain. Taasisi ya Wahat al-Qur'an al-Karim iliyoasisiwa Bahrain mwaka 1975 hivi sasa ina matawi 20 kote nchini humo ambapo madrasa 150 za Qur'ani na wanafunzi 1000 wa Qur'ani Tukufu wanaendeshea shughuli zao. 714316