IQNA

Usajili wa majina ya washiriki wa mafunzo ya usomaji Qur'ani kuanza kesho Niger

16:52 - December 21, 2010
Habari ID: 2051188
Usajili wa majina ya watu walio na hamu ya kushiriki katika masomo ya usomaji Qur'ani Tukufu ya mwaka ujao wa 2011 utaanza hapo kesho Jumatano katika mji mkuu wa Niger, Niamey.
Kwa mujibu wa tovuti ya actualite-islamique masomo hayo yanadhaminiwa na Kituo cha Kiislamu cha Niamey. Walio na hamu ya kushiriki kwenye masomo hayo wana muda wa kufikia Jumamosi Januari Mosi kusajili majina yao.
Masomo ya wanaume yataanza tarehe Pili na ya wanawake tarehe Tatu Januari katika kituo hicho mara tu baada ya swala ya Magharibi. Washiriki wanapasa kuwa na umri wa chini ya miaka 30 na wawe wanafahamu vizuri lugha za Kifaransa na Kiarabu. Ada ya masomo ni sharti jingine la kushiriki katika msomo hayo ya kila mwaka. 716046
captcha