Nuskha hiyo ya Qur'an ambayo inaaminika kuwa ya kale zaidi nchini China iliandikwa kwa mkono katika karne ya 8 au 9 Miladia.
Kwa mujibu wa gazeti la People's Daily la China, wataalamu wanasema Qur'ani hiyo iliingizwa China kutoka Asia ya Kati.
Kutokana na muundo wa jaladi lake, nakshi, muundo wa kaligrafia na karatasi, Qur'ani hiyo inahesabiwa kuwa moja ya nuskha za kale zaidi za Qur'ani Tukufu duniani.
716356