Akizungumzia suala hilo, Salim Abdul Jalil, mkuu anayesimamia masuala ya uhubiri katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri amesema kuwa msingi katika kutarjumiwa kitabu hicho kitakatifu ni kuwa mtarajumi anapasa kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na maana ya aya za kitabu hicho. Ameongeza kuwa kufahamu maana ya maneno pekee hakutoshi kumfanya mtu kuwa mtarjumi bora wa Qur'ani bali anapasa kufahamu vyema maana ya aya zake.
Amesema kwamba Wakristo hawana ufahamu mpana na wa kutosha wa aya zote za Qur'ani na kwa hivyo hawana uwezo wa kutarjumu vyema kitabu hicho kitakatifu.
Lugha ya Kiamazighi huzungumzwa kwa wingi na watu wa kaskazini mwa Afrika na hasa nchini Algeria. Tayari Qur'ani Tukufu imekwishatarjumiwa katika lugha hiyo na Haj Muhammad Tayyib, mwanafikra wa Kiislamu wa Algeria kwa ushirikiano wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya nchi hiyo, tarjumi ambayo inatazamiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni. 718795