IQNA

al Azhar yaainisha adhabu ya wanaopotosha Qur'ani na hadithi za Mtume (saw)

16:26 - January 01, 2011
Habari ID: 2056824
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar nchini Misri imependekeza adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela, faini ya lira elfu tano za Misri na kusimamishwa kazi miaka mitatu kwa taasisi yoyote ya uchapishaji itakayopotosha Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtume Muhammad (saw).
Gazeti la Misri la al Akhbar limeripoti kuwa mwaka 1985 Misri ilipasisha sheria ya 102 ambayo iliainisha adhabu kwa taasisi yoyote inayopotosha Qur'ani au hadithi za Mtume.
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar imerekebisha sheria hiyo na kuainisha kifungo cha miaka 15 jela, faini ya lira elfu 5 na kusimamishwa kazi miaka mitatu kama adhabu ya kupotosha Qur'ani Tukufu na hadithi za Mtume (saw).
Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar pia imeunda kamati ya kuchunguza kwa undani sheria hiyo mpya ambayo itachunuzwa katika kikao cha taasisi hiyo na kuwasilishwa katika bunge la Misri kwa ajili ya kupasishwa.
Wanachama wa taasisi hiyo pia wametoa wito wa kufanyika vikao vya masuala ya kiutamaduni katika mikoa mbalimbali ya Misri kwa ajili ya kukabiliana na fikra potofu za kisalafi na makundi yenye misimamo mikali ambayo yanalenga umoja wa Shia na Suni. 721733
captcha