IQNA

Wawakilishi wa Tanzania kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu

8:17 - January 05, 2011
Habari ID: 2059037
Wawakilishi wa Tanzania wanatazamiwa kushiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu yatakayofanyika siku chache zijazo katika mji mtakatifu wa Mash’had nchini Iran.
Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar es Salaam Tanzania ndicho kitakachosimamia safari ya wawakilishi hao na kushiriki kwao katika mashindano hayo.
Ibrahim Ramadhan Shaaban atashiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu katika uwanja wa kiraa huku mwenzake Hussein Abdullah akishiriki katika mashindano ya hifdhi ya Qur’ani nzima.
Washiriki hao kutoka Tanzania ambao ni wanafunzi wa chuo kikuu watachuana na wenzao kutoka nchi mbalimbali duniani katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yaliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 9 hadi 12 Januari.
Mashindano hayo yakayowashirikisha wanafunzi Waislamu wa Vyuo vikuu kutoka nchi mbalimbali duniani yanasimamiwa na Jumuiya ya Shughuli za Qur’ani ya Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran. 724110
captcha