IQNA

Ombi la kutengwa fedha zaidi kwa ajili ya taasisi za Qur'ani Gambia

14:17 - January 11, 2011
Habari ID: 2062698
Kituo kimoja cha hifdhi ya Qur'ani Tukufu nchini Gambia kimetaka kutengwa fedha zaidi kwa ajili ya kuzisaidia taasisi za Qur'ani za nchi hiyo ili ziweze kuhuisha sunna ya kuhifadhi Qur'ani na kuifikisha kwa vizazi vijavyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Today.gm Omar Darbou, Mkuu wa Kituo cha Hifdhi ya Qur'ani cha Ibrahim, aliyekuwa akizungumza mbele ya hadhara ya wazizi katika kikao cha baraza kuu cha kituo hicho, ambacho hufanyika kila mwaka, amesisitiza kwamba taasisi kama hizo zinapaswa kuungwa mkono kifedha na jamii. Amewataka wazazi kutuma watoto wao katika vituo hivyo sio kwa ajili ya kuhifadhi aya za Qur'ani tu bali kwa ajili pia ya kusoma na kujifunza maadili bora ya Kiislamu.
Huku akibainisha masikitiko yake kutokana na kutopewa umuhimu wa kutosha mafundisho ya Qur'ani, Darbou ametaka kufanyike juhudi zaidi kwa shabaha ya kueneza mafundisho ya Kiislamu katika jamii. Amesema kuna haja kubwa ya kuimarishwa ratiba na mipango ya kueneza Uislamu katika ngazi zote.
Katika kikao hicho, wananchi wa Gambia wametakiwa kutoa mchango wao katika kusaidia kuimarisha shughuli za shule za Kiarabu zinazowafundisha wanafunzi kuhifadhi Qur'ani na misingi ya dini. 728060
captcha