Mtandao wa "MyFoxOrlando" umeripoti kuwa Kasisi Terry Jones wa kanisa na Gainesville katika jimbo la Florida ambaye mwaka jana alitishia kuchoma kitabu kitakatifu cha Qur'ani na kuzusha wimbi kubwa la malalamiko duniani kote, sasa amechukua hatua nyingine na kuamua kuitisha siku ya kimataifa ya kuihukumu Qur'ani!
Amesema kesho Jumatano tarehe 13 Januari atafanya mkutano na waandishi habari katika mji wa Gainesville na kutoa maelezo zaidi kuhusu mpango wake ambao amepanga kuutekeleza katika siku za kuanzia tarehe 1 hadi 30 Machi mwaka huu.
Kasisi Jones amesema kwa mujibu wa mpango huo Waislamu wanapaswa kuthibitisha kwamba Qur'ani ni kitabu kinachohubiri amani! 729169