IQNA

Kituo cha uchapishaji Qur'ani cha Madina chalalamikia gharamu kubwa ya nuskha za Qur'ani

11:31 - January 13, 2011
Habari ID: 2063861
Kituo cha uchapishaji Qur'ani cha Mfalme Fahd katika mji mtakatifu wa Madina kimelalamikia vikali ughali wa nuskha za Qur'ani Tukufu unaofanywa na baadhi ya maduka ya mji huo na kuwataka viongozi husika wa serikali kukabiliana na jambo hilo.
Kwa mujibu wa Saudi Gazette, Muhammad Salim bin Shadid al-Aufi, katibu wa kituo hicho cha uchapishaji Qur'ani amesema kuwa baadhi ya maduka ya mji huo yanawauzia mahujaji na watalii nuskha za kitabu hicho kitakatifu kwa bei ya juu mno kuliko kiasi na kwamba yanatumia vibaya hali ya kutojua wengi wa wanunuzi wa nuskha hizo bei halisi wanayopaswa kutozwa. Ameongeza kuwa wauzaji hawapasi kuwatoza wanunuzi zaidi ya bei iliyoainishwa.
Huku akiashiria kwamba asilimia 98 ya nuskha zinazochapishwa na kituo hicho hutolewa bure kwa Waislamu kote ulimwenguni, al-Aufi amesema kuwa chini ya asilimia moja ya nuskha zinazochapishwa na kituo hicho huuzwa chini ya bei yake halisi. Amesema tayari kituo hicho kimechapisha nuskha za Qur'ani kwa lugha 50 tofauti ambazo zitatawanywa ulimwenguni katika kipindi cha miezi mitano ijayo na kwamba hivi karibuni lugha hizo zitaongezwa hadi kufikia 60. Amesema kituo hicho pia kinazalisha CD za tarjuma ya Qur'ani. 729292
captcha