IQNA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani, shakhsia bora wa Qur'ani

13:34 - January 15, 2011
Habari ID: 2064472
Kamati inayosimamia uchaguzi wa shakhsia bora wa Qur'ani nchini Qatar metangaza kwamba Abdallah Basifr, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimatifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu ndiye shakhsia bora wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiarabu katika mwaka uliopita wa 2010.
Geith bin Mubarak al-Kuwari, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Qatar pia amechaguliwa na kamati hiyo kuwa shakhsia bora wa Qur'ani nchini humo katika mwaka uliopita. Ibrahim Aali Ibrahim, mkuu wa Baraza la Kiidara la Darul Qur'an al-Karim ya Qatar amesema kuwa shakhsia hao wamechaguliwa baada ya kufanyika uchunguzi na vikao kadhaa vya kutathmini shughuli zao za Qur'ani. Amesema hafla ya kuwashukuru shakhsia hao ambayo itahudhuriwa na wakuu na wawakilishi wa taasisi na mashirika ya Qur'ani na tablighi kutoka nchi tofauti za dunia itafanyika tarehe 22 mwezi huu wa Januari.
Aali Ibrahim pia emesema kuwa duru ya kwanza ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani mashuhuri kwa jina la al-Usrat al–Hafidha ambayo iliyoanza Januari 9 kwa udhamini wa Darul Qur'an al-Karim, inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar ilikamilika tarehe 11 Januari. 730124
captcha